DYNA ATOA SABABU ZA KUPOST PICHA ZA MWONEKANO WAKE KIMAHABA KWENYE ACCOUNT YAKE YA INSTAGRAM.

Ilikuwa nadra sana kwa Dyna kuonekana katika picha na pozi zenye utata kama hizi labda ndiyo sababu ya kila mtu kuchukulia kivyake.

Baadhi ya mashabiki waliponda na wengine wakichukulia poa lakini kwa mujibu wa dyna mwenyewe anasema wachache tu ndo waliokerwa na picha hizo.

Kupitia Planetbongo dayna amesema watu hawatakiwi kushtushwa na picha hizo kwani yeye ni msanii na haiwezekani afanye jambo kama hilo bila sababu ya msingi.

Hakuweka wazi sababu hiyo akisema ni mapema kwa sasa kusema lakini watu waelewe tu, amefanya hivyo akiwa na sababu maalum.

Tujikumbushe..

Malkia wa muziki, Dayna Nyange aliamua
kuwaonyesha mashabiki wake laki moja na
ishirini wa instagram mwonekano wake wa
kimahaba.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Komela’ akiwa na Billnas, Jumanne hii amewatoa udenda mashabiki wake kwa picha hizo za kuvutia.

Huwenda yakawa ni maandalizi na video mpya, lakini mwanadada huyo hakuweka wazi ni nini kinakuja kutoka kwake. hilo nimoja ya swali tulilokuwa tunajiuliza watu wengi.

Hope, zitakuwa hazijakupita picha hizo.

IMG-20160921-WA0011


IMG-20160921-WA0010

IMG-20160921-WA0007

Story By: @Joplus_

Source: Perfect255.com