Dj Khaled na Diddy wafululiza Party.

Mtoto wa kwanza wa kiume wa Mfalme wa mtandao wa Snapchat, Rapa, Mtangazaji na Dj ‘Dj Khaled’, Asahd Tuck Khaled tarehe ya leo ametimiza umri wa mwaka mmoja na sherehe za hatua hii ya umri zilianza siku ya Jumamosi ukumbi wa LIV nightclub unaopatikana Fountainebleu huko mjini Miami.

Sherehe hiyo ya siku kubwa ya Asahd Khaled ilipambwa na burudani ya staa wa muziki wa rap, mfanyabiashara na rafiki wa karibu wa Baba yake na Asahd (Dj Khaled), P Diddy na maoni ya wengi wao walioudhuria tukio hilo la Birthday Party walikiri kuwa siku hiyo iliendeshwa kwa burudani kubwa ya aina yake.

Sherehe hiyo ilikuwa ni mwanzo tu kwakuwa mara baada ya burudani katika ukumbi huo sherehe iliendelea sambamba na chakula cha jioni(After Party) katika Mgahawa maarufu ‘Komodo Restaurant.’

Asahd Khaled ni mchango mkubwa katika Album ya kumi ya Dj Khaled ‘Grateful’ iliyotoka rasmi Mwezi Juni mwaka huu kwa kupewa nafasi kubwa ya utayarishaji wa album hata kuwa pambo la cover ya album hiyo.

Source: Dizzim online.