DIAMOND Platnumz Awashukia Wanaojifanya Wajuaji wa Muziki

Msanii Diamond Platnumz Jana Mei mosi ameamua kuwatumia ujumbe wasanii wenzake kwenye bongofleva kwa kuwaandikia kupitia ukurasa wake wa Instagram ushauri wake kwao ili waweze kufanya vizuri kwenye masoko ya nje.

“Leo ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa… Siku hizi mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu….pasipo kujua kuwa kila nyimbo ina soko lake na kila mwanamziki anapotoa nyimbo anakuwa na malengo ama plan ambayo kaidhamilia…leo ntakupostia baadhi ya nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na wanaojifanya wajuaji wa Muziki… pasipo kujua kuwa dhamira ama nini yalikuwa malengo yangu….kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani….. sababu yangu kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia…lakini pia kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda, hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina “UKIMUONA” Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine… #SimbaInZambia

 Source: Udaku