BOB JUNIOR AMTOLEA POVU JOSE CHAMELEONEKWA SABABU YA VIDEO YAO.

Producer na muimbaji tokea Sharobaro Records, Bob Junior amemchana mkali tokea pande za Uganda, Jose Chameleone baaa ya kufanya wimbo pamoja ambao video yake haijatoka, wimbo unaofahamika kwa jina la “Siachani Naye” mwanzoni mwa mwaka huu.

Bob Junior alidai kuwa alikuwa na nia ya kufanya video ya wimbo huo lakini kila alipokuwa anapanga ratiba za ku’shoot, Chameleone
alikuwa akikwepa.

Akipiga story na eNewz Bob Junior alisema “Tukipanga siku ya ku’shoot, ikifika siku hiyo nikimtafuta basi hajibu meseji zangu, sasa mimi nitafanyaje? Hata hivyo sitaki kusema mengi kwa ubaya, labda kuna vitu kweli vinamzuia”.

Hata hivyo Bob Junior alisema baada ya kushindwa kufanikisha kufanya video hiyo, sasa anajipanga kwa kazi nyingine, huku akisema anatarajia kuachia wimbo alioshirikiana na Q Chief na Baraka da Prince, wimbo unaoitwa “Kidege” na kama si wimbo huo basi ataachia mwengine unaoitwa “Mpasuo”.

Story By:@Joplus_

Source: Udaku Special Blog