AY aeleza alichokiona kwa Sallam hadi amshawishi awe meneja wa muziki

Hivi unafahamu AY ndiye mtu wa kwanza kumuona Sallam SK kuwa anafaa kuwa meneja wa muziki? Kwa sasa Sallam anafahamika zaidi kama meneja wa Diamond na AY pia.

Akiongea na XXL ya Clouds FM kupitia 255, AY alisema, “Ni kweli mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kumuona pia Sallam SK, alikuwa anafanya kazi bandarini ni mtu aggressive, mchapakazi na anapenda kufuatilia vitu. Nikaona hatuna watu wa hivi kwenye industry nikaona kwanini tusimpatie nafasi.”

AY aliongeza, “Kilichonivutia zaidi ni ile kuwa aggressive, kuwa mtafutaji, kuwa mpambanaji akiamua kukitafuta kitu anakitafuta kwa njia yoyote na nikaona ni mtu mmoja wapo anayeweza kusaidia muziki kupiga hatua. Pia kwenye industry tunatamani watu wengine 10 kama hao ili muziki wetu kwenda mbali na kuweza kuupush muziki wetu pia tunahitaji watu wa namna hii kuweza kugawana mapato.”

Source: Dizzimonline