Alichozungumza Steve Nyerere kuhusu Bongo movie kuandamana

Headlines za waigizaji wa Bongo movie kuandamana wakitaka usitishwaji wa filamu za nje hapa nchini kwa lengo la kuinua soko la filamu za ndani limewagusa wadau mbalimbali hasa wasanii wengine wa tasnia hiyo.

Leo April 26, 2017 mmoja wa mastaa wa tasnia hiyo walioguswa na tukio hilo na kueleza mtazamo wake ni Steve Nyerere ambaye amekuwa na mtazamo tofauti na mastaa wengine wa tasnia hiyo akisema kuwa zilipaswa kufuatwa njia sahihi katika kulitatua tatizo lao na siyo kuandamana hadi Kariakoo kwa Wamachinga.

Ayo TV Entertainment na millardayo.com imepiga stori na Steve Nyerere na moja ya mambo aliyoyagusia katika sakat hilo ni namna lilivyofanyika.

“Hatukutakiwa kutoka hapa na malori, tulitakiwa tukae chini tujue tunalisolve vipi hili. Tulitakiwa tukae na wasambazaji siyo Machinga.” – Steve Nyerere.

Source: Millard ayo