Â
Miss Tanzania 2-16 Diana Edward ameongea baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aliyoahidiwa kwenye mashindayo hayo yaliyofanyika October 2016.
Diana amesema hakukata tamaa kuhusu kuisubiria zawadi yake hata kama imechukua miezi 6 baada ya fainali yenyewe kufanyika na kwamba hata yeye hajui ilikuaje japo wakati wa shindano kuna gari lilionyeshwa kwamba ndio ilikua zawadi yenyewe.
‘Nilikua nategemea kupata gari dogo lakini sijui ni aina gani… na kuhusu kuchelewa kupata zawadi siwezi kulaumu sana kwasababu kila mtu anajua sasa hivi uchumi wa nchi umeshuka, namshukuru Mungu tu‘
Source: Millard ayo