Wolper Aisifia Couple Ya Navy Kenzo.

Star wa Bongo Movie, Jackline Wolper, amesema uhusiano wa wasanii wenzake, Aika na Nahreel, wanaounda kundi la muziki la Navy Kenzo, ndiyo ‘couple’ imara zaidi kwa wasanii kwa sasa. Wolper alisema anafurahishwa na wanavyoweza kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika uhusiano wao na hawayumbishwi licha ya kuwa mastaa wakubwa kwa sasa katika muziki. “Wamejitahidi sana kudumisha mapenzi yao, wamenifanya niwaone ndiyo couple imara na inayokubalika kwa sasa ukitofautisha na wasanii wengine,” alisema Wolper. Hata hivyo, Wolper ambaye kwa sasa yupo kwenye uhusiano na msanii kutoka kundi la WCB anayejulikana kwa jina la Harmonize, amesema uhusiano wa wasanii hao unampa funzo kubwa katika maisha yake ya uhusiano huku akiahidi kufuata nyayo zao. Wasanii wapenzi hao wanaounda kundi la Navy Kenzo, walinukuliwa hivi karibuni wakisema kwamba wanapokwazana na kutaka kuachana hufikiria ugumu waliopitia walipokuwa wakitengeneza majina yao na namna watakavyokuja kuyapoteza kirahisi.

Source: Dizzim Online.