Wezi wamliza Barnaba, Wampora begi lililokuwa na vitu vya thamani

Mkali wa ‘Lonely’ ameianza wiki vibaya baada ya wezi kumpora begi lake lililokuwa na vitu vyake vya muhimu ikiwemo Passport ya kusafilia, Laptop mbili, Hard disc zenye kazi zake na mikataba na camera.

Kupitia Instagram Branba ameandika ujumbe huu,

“Za asubui Ndugu Zangu wapendwa Usiku wa kuamkia Leo Nimeibiwa Begi langu Dogo Tu si Kubwa Sana ambalo lilikuwa ndani ya Gari langu | lakini ndani Yake Kulikua Na Laptop 💻 za mac mbili moja Pro x moja Letina ya ukubwa Kidogo Theni Kuna external mbili moja Rangi Ya orange 🍊 moja Ya kijani Na Kuna File Zangu zilikua Na Mikataba Mbali Mbali lakini Kikubwa zaidi Ndani Yake Kuna PASPORT Yangu ambayo Ukifungua ndani Inasoma Jina La ELIASI BARNABASI INYASI and Kuna Vitu Vingi Sana Vidogo vidogo Vyenye Thamani Kubwa Kama Camera 🎥Na vingine Lakini Naomba sana Sana Waungwana Kama Kuna mtu Yotote atabaini au kujua Vilipo au hata kupelekewa Basi Naomba wasamalia Wema mnirudishie Au kuniletea Na Napatikana kwa No 0743505010 Mungu Awabariki Na naamini Aliyenavyo ajaiba Bali amepitiwa katika njia ya kutafuta Ridhiki Nami kwa jina la mungu nitamsamehe Na nimesamehe ila Kama Ana Rohoo nzuri Na ameguswa Basi Naomba waungwana mnipigie hata Kama Umeokota 😰😭”

Source: Teentz