Watu wa Nyumba Yako

Ni sunnah kuwawia wana nyumba wako kwa wema kabla ya kutoa sadaka kwa watu wa nje.

1. Al Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. siku moja aliwasaidia waombaji watatu na wa nne alipokuja hakumpa chochote. Na hapo Al Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. akasema:
“Iwapo mtu atakuwa na Dirham elfu thelathini au arobaini na zote akazigawa kwa kusaidia au sadaka bila ya kubakiza chochote kwa ajili ya wana nyumba wake basi huyo mtu atakuwa mmoja miongoni mwa watu watatu ambao dua zao hazikubaliwi na Allah swt. Na katika watu hawa watatu: mmoja ni yule ambaye bila kutimiza wajibu wake anagawa mali yote kama sadaka au kusaidia, na baada ya hapo anakaa akiomba dua:
“Ewe Allah swt naomba unipe riziki.”
Basi hapo atajibiwa, “Je! mimi nilikuwa sikukufanyia njia ya kujipatia riziki?”

2. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:
“Bora ya sadaka zote ni ile inayotolewa wakati mtu anapokuwa na uwezo wa kutoa yaani katika hali ya utajiri na unapokuwa sawa.”

3. Hisham bin Al Muthanna anasema:
“Kuna mtu mmoja alimwuliza Al Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. kuhusu tafsiri ya ayah Surah An-a’am, 6, Ayah 141:
‘Na Yeye ndiye aliyeziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.’

Al Imam Ja’afer as-Sadiq a.s. alimjibu,
“Katika Ansaar alikuwako mtu mmoja (aliwapa jina lao) ambaye alikuwa ana shamba. Pale mazao yake yalipokuwa yakiwa tayari yeye alikuwa akigawa yote katika sadaka, na alikuwa hawapi chochote watoto na wana nyumba yake; na kwa tendo lake hili Allah swt alikuwa akimhesabia yeye kama ni mfujaji na mbadhirifu.”

story@moodyhamza