Mwingine Yamoto Band atoka kivyake, vipi kuhusu kundi?


Zikiwa zimepita siku chache tu tangu mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Yamoto Band Aslay kuachia wimbo binfasi unaoitwa ‘Angekuona’ kitendo kilichotafsiriwa kuwa mwanzo wa kuvunjika kundi hilo, sasa msanii mwingine ameamua kutoka kivyake.

Leo staa mwingine wa kundi hilo Beka Flavour ameachia wimbo wake mpya ambao unaitwa ‘Libebe’ akisema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuonesha uwezo binafsi:“Huu wimbo ni nje ya kundi la Yamoto Band. Lengo ni kuonyesha uwezo binafsi kwetu sisi. Ameanza Aslay, sasa ni zamu yangu.” – Beka Flavor

                                                   Source: Millard ayo