Mwimbaji Lulu Diva Amwanika Mpenzi wake mpya.


BAADA ya kuweka hadharani kuwa amepata meneja mpya katika za muziki, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kutoka kimapenzi na meneja huyo ambaye pia ni mwanamuziki kutoka Kenya, Jaguar.
Kwa mujibu wa chanzo, hivi sasa mrembo huyo amejiweka kwa Jaguar na hivi karibuni alipewa kipondo na bwana’ke wa zamani baana ya kubaini uhusiano huo.

 

“Safari zake Kenya zimekuwa haziishi, wenyewe wanadai wapo kikazi lakini mhh si kwa mapozi ya kimahaba wanayoonesha,” kilibonyeza chanzo na kuahidi kuwabofya picha akiwaona tena.
Baada ya kunasa madai hayo, Star Mix lilimtafuta Lulu na alipopatikana alisema;
“Ni uzushi kama unavyojua Wabongo, Jaguar ni meneja wangu tu ambaye ananisaidia katika kunisimamia katika muziki na si vinginevyo.”

Source: Udaku