Mashabiki wa Ali Kiba Sio Real Ni Maadui.


Mchekeshaji kutoka Timamu, Mama Ashura amesema hakuumizwa na maneno makali katika mitandao ya kijamii kutoka kwa mashabiki wa Alikiba baada ya kumkosoa msanii huyo kwa kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo.

Mwaka huu alikosoa vikali utaraibu wa Alikiba kukaa kipindi kirefu bila kutoa wimbo kitu ambacho kilipelekea kushambuliwa kwa maneno makali na team Kiba.

“Hao mashabiki Alikiba mwenyewe hawajui, halafu hawapi hata sapoti, mashiki wa Alikiba siyo wale real kabisa ni maadui wa Diamond,” amesema.

“Wanakuja kwa upande wa Alikiba wao wana-take advantage ya kumsapoti huyo ambaye yupo tofauti na huyu lakini wangekuwa real wasingekuwa wanatumia matusi.

Katika hatua nyingine alimtaja Alikiba kama msanii asiyeonyesha ushirikiano kwa mashabiki wake na wale wanaomsapoti katika mitandao ya kijamii.

“Eric Omondi alitoa cover ya Zilipendwa na Seduce Me, Diamond alicomment ‘asante’ lakini Alikiba!!!! (hakufanya hivyo)” amesema.

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!