Kutana na msanii mpya kwenye label ya Vanessa Mdee

Vanessa Mdee amemtambulisha msanii mpya kwenye label yake ya Mdee Music ambayo awali alikuwepo yeye pamoja na mdogo wake ambaye ni Mimi Mars. Msanii huyo ni rapper na anaitwa Brian Simba a.k.a Jamaa Flani.

Vanessa amemuelezea Brian Simba kama kijana mwenye nidhamu ya kazi na tangu alipomuona kwa mara ya kwanza aliona kuwa ana kipaji kikubwa ila anachohitaji ni mtu wa kumsaidia afike mbali na hiyo ndiyo sababu ya kumsaini kwenye label yake ya Mdee Music.

                                                              Source: Millard ayo