Fid Q Afunguka Remix ya Wimbo Wake.


Rapa Fid Q amefunguka na kuonyesha hisia zake juu ya mambo mbalimbali ambayo yametokea baada ya moja ya msanii wa bongo kufanya ‘Remix’ ya wimbo wake ‘Fresh’ na kusema yeye mwenyewe alikuwa hajui kama msanii huyo alimchana hasimu wake Alikiba.

Fid Q amedai kuwa yeye si mfuatiliaji wa muziki wa bongo fleva hivyo kuna mambo mengi kuwahusu wasanii hao hayajui na kudai hata aliposikia kwenye ‘Remix’ hiyo neno Cinderela alijua kuwa amemaanisha ni mwanamke na kudai hakufikiri wala kuwaza kama lilikuwa ni dongo kwa Alikiba.
“Aliposema ule mstari sijui msinifananishe na Cinderela mimi nilichukulia ile Cinderela kama usinifananishe na mtoto wa kike, niwakumbushe mimi ni mtu wa hip hop sijui chochote kile kuhusu bongo fleva, najua majina ya wasanii wa bongo fleva ila sijui chochote kuhusu miziki yao, hivyo kile alichoimba ni hisia zake yeye kwa hiyo niseme tu mimi mwenyewe nilifichiwa ‘white’ sikujua ile Cinderela iliyoimbwa mle ni wimbo wa Alikiba na sikujua kama ni dongo kwa Alikiba” alisema Fid Q

Aidha Fid Q amedai kutokana na kile alichofanya Ommy Dimpoz kupitia mtandao wake wa Instgram kujibu ile ngoma kimemuondolea vibe kabisaa na kudai saizi hata ukimuuliza ‘Fresh’ yeye atakwambia siyo ‘Fresh’, mbali na hilo Fid Q amesema ndoto yake sasa ni kuona anakuja kuwakutanisha wasanii hao wawili ili waweze kumaliza hizo tofauti zao kwa sababu yeye wote yuko nao sawa na hana tatizo nao.

Source: Udaku

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors