Wanasayansi kutoka Swansea University, Uingereza wamegundua bandeji zinazojulikana kama ‘Smart bandage’ ambazo pindi anapofungwa mgonjwa hupeleka taarifa moja kwa moja kwa daktari hata kama mgonjwa huyo yuko nyumbani.
Bandeji hizo zinazotumia mfumo wa 5G zimewekwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kupima hali ya maumivu ya mgonjwa na kupeleka taarifa kwa daktari bila ya mgonjwa kwenda hospitali ambapo kwa mujibu wa Daktari Marc Clement, bandeji hizo zitaanza kutumika rasmi mapema mwaka 2018.
Source: Millard ayo