Duniani Sababu za kwanini Wanandoa wengi hufanana

Ni miongoni mwa swali wanalojiuliza watu wengi kwanini Wanandoa wengi hufanana? sasa leo nimekuletea majibu ambapo Wanasayansi wa chuo kikuu Boston Marekani wamefanya uchunguzi na kugundua sababu kubwa ya wanandoa kufanana ni kuoa watu wanaoshea historia ya undugu mfano watu wa kabila moja.

Rapa Dj khalid na mke wake Nicole Tuck

Wanasayansi hao wamesema kitendo cha watu kwenda kuoa au kuolewa kwenye miji au vijiji walikotokea kuna changia Wanandoa wengi kujikuta wana sura zinazofanana kutokana na makabila mengi kuwa na sifa moja inayofanana mfano pua nyembaba, pua kubwa, macho madogo n.k


Sababu nyingine waliyoitoa ya kwanini Wanandoa wengine sio kabila moja lakini bado wanafanana, wanasema kwa kawaida ubongo wa binadamu huwa na hali ya kumuamini mtu ambaye anavitu vinavyoendana na yeye na hali hii hupelekea watu kuoa au kuolewa na watu wanaofana vitu.

Staa wa 50 shades of grey Benedict Cumberbatch na Mke wake

Akielezea sababu ya kwanini wanandoa ambao walikua hawafanani hapo kabla kuanza kufanana baada ya miaka mingi kwenye ndoa, Mwanasaikolojia Robert Zajonc alisema jinsi wanandoa wanavyoishi inapelekea kufanana mfano Mwanaume anaye kasirika sana hutengeza mikunjo kwenye uso wake na Mwanaume wa aina hii humkasirisha mke wake pia ambaye naye atatengeza mikunjo ya uso hivyo kujikuta wamefanana.

 Source: Millard ayo