Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na mmoja wa wanandoa kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa bila kujua kuwa vipo vyakula tunavyokula vinavyoweza kuchangia rekebisha tatizo hilo ndani ya miili yetu .
Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na hivi hapa chini vifuatavyo:
1. Karanga
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya. Mzunguko mzuri wa damu katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri na kulifurahia.
Pamoja na hayo, karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.
2. Tangawizi
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi inasifika kwa kuwa na uwezo wa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume.
3. Asali
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
4. Pilipili
Pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamsha haraka hisia za mapenzi na pia usaidia mwili kuwa na hisia za haraka zaidi kwa kuguswa na kadhalika.
5. Matunda & mboga za majani
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi.
                                 Source: Udaku