DULLY SYKES AKIRI KUWA ILI UWE MAARUFU LAZIMA UANDIKIWE NYIMBO.

Hit maker wa ngoma wa “Inde” ambaye ni Legendary wa muziki huu wa Bongo Fleva Prince Dully Sykesa.k.a Brother Man amefunguka kuwa ili uweze kuwa Legendary ni lazima upitie hatua ya kuandikiwa nyimbo.
Dully Sykes ametolea mfano kwa wanamuziki wakubwa duniani kama Michael Jackson ambao nao pia wamewahi kuandikiwa nyimbo na zikafanya vizuri. Dully Sykes anadai kuwa kuandikiwa nyimbo sio udhaifu bali ni kujipima uwezo wako kama unaweza kutembea kwenye mawazo ya watu wengine.
Dully Sykes ameiambia P
kuwa nyimbo ya “Inde” amesaidiwa kuandika na msanii Raymond wa WCB.
“Inde nimesaidiwa kuandika na Raymond, ngoma nyingine ambayo nimeandikiwa ni Dhahabu. Kwenye nyimbo hiyo chorus niliandika mwenyewe ila verse nilisaidiwa na msanii anaitwa Jay C.” Alisema Dully Sykes
“Me napenda kuandikiwa nyimbo, na hakuna Legend ambaye hajawahi kuandikiwa, na pia huwezi kuwa Legend kama hujawahi kuandikiwa, kwasababu legend si mjivuni.” Hayo ni baadhi ya maneno ambayoDully Sykes aliyaongeza pamoja na mengine meengi ambayo nimekuwekea hap chini kwenye hii video. Itazame

Story by:@Joplus_
Source:Raha za walimwengu.