Maswali ya watu wengi ilikua ni kujua msanii gani au ni jamaa gani aliepata nafasi ya kusainiwa kuwa wa kwanza kwenye label ya ‘Mgumu’ Fid Q baada ya taarifa ya awali kutoka kuwa Ijumaa ya leo atamtambulisha msanii wake wa kwanza kutoka label ya Cheusi Dawa.
Sasa majibu tunayo hapa kutoka kwa Fid Q mwenyewe ambaye amesema kuwa ameamua kumsaini Big Jah Man kwenye label hiyo ya Cheusi Dawa na kitu kizuri ni kuwa wameachia na wimbo wa pamoja unaitwa Mabundi.
Big Jahman
Mussa Loth Kaaya aka Big Jahman ni msanii wa dancehall wa siku nyingi ambae anatokea mkoa wa Arusha na amepata zali la kuwa msanii wa kwanza wa label hiyo,wimbo wanaouachia leo umetayarishwa na producer mchanga aitwaye Star Jay na kwa upande wa mastering imefanywa na P-Funk Majani kutoka Bongo Records.
Source: Dizzim online