HIT maker wa ngoma ya Wasikudanganye, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa anavutiwa na kila kitu ambacho wasanii wenzake wawili; Dogo Janja na Billnas hivyo kwake yeye, hao ndiyo chaguo lake.
Akizungumza na Showbiz Extra, Nandy alisema, mbali na kwamba wasanii hao kuwa washkaji zake wa karibu na kuhusishwa nao na skendo za mapenzi lakini uwezo wao katika kazi unamfanya kuwa shabiki namba moja wa waimbaji hao.
“Kwa Billnas na Dogo Janja huniambii chochote, kwa hapa Bongo hao ndiyo wasanii wangu bora, napenda kile wanachofanya cheki wanavyovaa, cheki muziki wao, cheki wanavyojua kwenda na wakati, kwa kweli sina sababu ya kutowashabikia ingawa nimekuwa nikihusishwa kutoka nao kimapenzi lakini hakuna ukweli wowote,” alisema Nandy.
Source: Udaku.