April 25 2017 Msanii wa Filamu nchini Jacob Steven maarufu kama JB’ amefunguka kuhusiana na swala la baadhi ya wasanii wa bongo fleva kutoa mtazamo wao wa tofauti kuhusu bongo movie, ambapo alipoulizwa na mtangazaji wa Enewz jinsi alivyopokea kauli ya Rapa Nay wa Mitego ya kuwaponda wasanii wafilamu waliondamana.
JB’ amesema kuwa yeye ni mkristo na hajafunzwa kutukana na anawapenda bongo fleva japo hafatiliagi na istoshe akisema hamfahamu msanii watu wasije kuona anatania kwa sababu hakuwai kusikiliza nyimbo ya msanii huyo na hatakama kasema hivyo yeye bado anampenda na kusisitiza kwa kusema unachokiona nyama mwenzio anaweza kukiona sumu…
..>>> “Mwalimu wangu wa Economics wakati nasoma form five na form six alinifundisha msemo mmoja One man’s meat could be another man poison’ wewe unaweza kuona hii nyama mwenzio akaona hii sumu kama wao wametuona sisi matahira sisi tunawashukuru na Mungu awabariki sana” – JB’
“Mimi ni Mkristo sijafunzwa kutukana nimefunzwa kuwapenda watu wote na kuwaheshimu tunawapenda sana bongo fleva ingawa mara nyingi mimi siangaliagi na kwa kutokusikiliza Bongo fleva haina maana kwamba siwakubali na siwapendi”
“Nikisema kwamba simfahamu watu wengine wanao niangalia wanaweza kuona kama natania sijawai kusikiliza nyimbo yake kwahiyo siamini kama ni mwanamziki kweli amesema labda ungenionyesha ni huyu ningeweza kujibu na hata kama amesema mimi nampenda na hayo ni maoni yake, kitu mtu anachosema huwezi kumbishia ila sisi tunawapenda sana wenzetu wa bongo fleva”
“Niuwongo kusema kwamba tunataka zile muvi za nje zisiwepo hapana, tunachotaka sisi ni wafate utaratibu kama sisi tunavyofanya aidha wao wafate taratibu au nasisi tusifate utaratibu” JB’
Source: Millard ayo