MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa kwenye Hip Hop Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amewaka kwa kusema kuwa, wanaoiponda ngoma yake mpya anayotegemea kuachia hivi karibuni iitwayo Govinda ni watu ambao hawapendi maendeleo yake lakini atawanyamazisha mdomo baada ya kuiachia.
Muda mchache baada ya kusambaza kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii cha wimbo huo mpya na kukutana na changamoto za watu kuiponda ngoma hiyo na kumwambia anatakiwa kubadilisha namna ya ufanyaji wake wa kazi Chid alisema;
“Bado nina watu wengi wanaoufuatilia muziki wangu na wanapenda namna ninachana kwa hiyo hata siwezi kusikiliza maneno ya wachache ambao hawanipendi wanaoponda ngoma yangu, kikubwa mashabiki wategemee kupata vitu vikali zaidi kutoka kwangu maana kwa sasa nilishabadilika na kuwa mtu mpya.
Source: Udaku.