Ikiwa zimepita siku nane toka rapa maarufu wa Marekani Rick Ross ampost Staa wa Bongo Diamond Platnumz katika ukurasa wake wa Instagram kwa mara ya kwanza akiwa amebeba chupa za kinywaji cha Belere ikiwa ni ishara ya kukinadi kinywaji hicho, usiku wa September 17 amempost tena.
Diamond ni balozi wa kinywaji hicho cha Belere na yeye amekua Staa wa pili kutoka Afrika kupostiwa na Rick Ross baada ya siku kadhaa zilizopita mwanadada kutoka nchini Kenya Huddah Monroe pia kupata bahati hiyo ya kupostiwa na Staa huyu wa Hollywood.
Source: Millard ayo.