Yuzzo – Hii Ni Hip Hop – (Video)

Toka studio za Perfect Tree Records chini ya mkono wa “Diego Lopez” Hip-hop Soldier Yuzzo toka Watengwa Tanzania mwenye maskani yake Ulaya kwa sasa anakujia na official video ya ngoma yake mpya kwa jina “HII NI HIP-HOP” Enjoy

LYRICS: Hii Ni Hip Hop

Intro: Worldwide Hip Hop

Chorus 1

Hii Ni Hip Hop Kwanza Unaburudika
Busara Na Slung Za Mtaa Zinasikika
Alaf Chambua Kisha Thaminisha
Kama Imekubamba Basi Tingisha Kichwa

Verse 1

Check It Out Yoo Yuzzo
Napenda Kutunza Misingi Sio Kushindana
Mjasilia Shuhuda Wa Mitaa Ya Kifukara
Misala Frustration Depression Na Vibaka
Kwetu Wametoka Mastaa Mtaa Walioukana
Makahaba Na Manyamara Usije Kifala
Sikai Kiree Ebu Nipate Maabara
Najitambua Natambua Nyakati Na Ishara
Siwezi Rap Anasa Nilipotoka Majanga
Slum Bure Antibiotics Unanipata
Emmune System Chini Na Maafa
Conspiracy Medical Industries Tunasafa
Dini Siasa Uchaguzi Tunachinjana
Wenye Uchu Wamedhamiria Ya Kinyama
Yasiyo Simulika Kuliko Waliyo Aanika
Hardcore Rapper Ladha Old-school Bila Mashaka
Navuka Mipaka Nazidi Kukipaka
No Shanapa Hapa Usilete Dhihaka
Brother Kaka Mwambie Hata Dada
This is Gideon Time Tuijenge Africa
Reasoning Mh Nguvu Inahitajika

Chorus 2

Hii Ni Hip Hop Kwanza Unaburudika
Busara Na Slung Za Mtaa Zinasikika
Alaf Chambua Kisha Thaminisha
Kama Imekubamba Basi Tingisha Kichwa

Verse 2

Acha Mapepe Nikupe Issue Serious
Nazidi Kusaka Solution Kupinga Inferiors
Niko Focus Na Vouchers Wanavyovizia
Ndoto Za Maisha Rough Hatujasinzia
Mafumbo Na Udharimu Wa Walafi Tunavumilia
Urasimu Unatesa Mjane Yatima Wasiohatia
Vifo Watoto Na Chanjo Ya Kuzingatia
Eeh Jombaa Sijawahi Jikomba
Kichwani Natty Konga
Nadunga Verse Noma
Sipretend Sikiza Mistari Yangu Nahau
Africa Myth-ology Desturi Sijasahau
Black Phylosoph Confidence Mila Nidhamu
Lyrical Technical Ghetto Naongeza Wadau
Mafao Ya Mnyonge Vipi Au Nimwage Damu
Salam Za Shujaa Timamu Karam Futa Haram
Hatamu Mimi Timamu Kichwani Ni Chakaramu
Tungo Bado Zinaweza Tunga Filamu
Ghetto Mpaka Downtown Natuma Ujumbe Kwa Sound
Check Skiza Hii Sound Ya Boombap Yuzzo Na Diego Kwenye Beat

Chorus 3

Hii Ni Hip Hop Kwanza Unaburudika
Busara Na Slang Za Mtaa Zinasikika
Alaf Chambua Kisha Thaminisha
Kama Imekubamba Basi Tingisha Kichwa (x2)
Swahili Hip Hop