Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa

ZIFAHAMU FAIDA ZA MIWA NA JUICE YAKE.

Inafurahisha kuona kuwa wapo
wafanyabiashara wengi jijini Dar es
Salaam na sehemu nyingi nchini wanaouza juisi ya miwa ama miwa yenyewe.

Kimsingi juisi hii ni sukari halisia
ambayo haijachakatwa. Sukari
halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina
virutubisho na madini kwa wingi.

Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi
ya miwa inafahamika na wataalamu
wa afya kwa kuwa na uwezo wa
kuupa mwili nguvu kwa sababu ya
‘glucose’ iliyopo.

Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina
kalori 11. Madini halisi na vitamin
zinazopatikana katika sukari ni
kama phosphorus, calcium, madini
ya chuma na potassium.

Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda
lenye alkali hivyo lina uwezo wa
kupambana na saratani hasa ile ya
kibofu cha mkojo na saratani ya
maziwa.

Miwa ina upekee wake kwani ina
uwezo wa kuongeza maji mwilini,
inaupooza mwili na kuupa nguvu.

Virutubisho vilivyopo katika miwa
vina manufaa makubwa katika
kusaidia utendaji kazi wa ogani
muhimu kama figo, moyo, ubongo na
viungo vya uzazi.

Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie
sukari iliyopo kwenye miwa kwani
haina madhara yoyote kwao. Uzuri
wa juisi ya miwa ni kuwa sukari
yake ni halisia.

story@moodyhamza