Ishu viongozi wa kisiasa na wafanya biashara kutoa maoni yao juu ya namna walivyoupokea wimbo mpya ‘Seduce Me’ wa mwimbaji Alikiba imezidi kuchuua headlines baada ya mwanasiasa na mwanasheria ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu naye kuwa mmoja wao.
Lissu ambaye ni Rais wa TLS leo August 29, 2017 kupitia twitter aliandika ujumbe ambao unaonesha kama kijembe kwa team ya WCB inayoongozwa na Diamond Platnumz akiandika Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme”
Source: Millard ayo.