Manuwari ya jeshi la Marekani uso kwa uso na ya Japan

Meli ya jeshi la Marekani ilikumbwa na uharibfui kidogo baada ya kugongana na chombo kingini cha Japan pwani ya Japan.

Chombo hicho cha kibiashara kilikosa mwelekeo na kuigonga manowari hiyo ya Marekani ya USS Benfold eneo la Sagami Bay.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenyo vyombo hivyo viwili, jeshi la Marekani lilisema na kuongeza kuwa uchunguzi unafanyika.

Katika taarifa jeshi la majini la Marekani lilisema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu kidogo,

Mwezi Agosti wanajeshi 10 wa Marekani waliuwa wakati Manowari ya USS John S McCain, iligongana na meli ya kubeba maftua nchini Singapore.

Mwezi Junuari wanajeshi 7 wa Marekani waliuawa wakati Manowari ya Marekani ya USS Fitzgerald, iligongana na meli ya mizigo kwenye maji ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.

@moodyhamza

Facebook Notice for EU! You need to login to view and post FB Comments!