Tma Yatoa Tahadhari Mvua Kuanza Mwezi Novemba.


MAENEO ya kusini-magharibi mwa nchi yanategemewa kuanza kupata mvua za masika kuanzia mwezi  Novemba mwaka huu hadi Aprili mwaka kesho (2018).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi, aliyesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alisema kutokana na mifumo ya hali ya hewa, mvua zitakuwa ni za wastani hadi juu ya wastani.
Kwa upande wa Kanda ya Magharibi ambayo inajumuisha mikoa ya Tabora, Rukwa, Katavi na Kigoma, mvua zitaanza wiki ya kwanza ya Novemba na kuendelea hadi wiki ya nne Aprili mwaka kesho. Kwa Kanda ya Kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma, mvua zitaanza wiki ya kwanza ya Novemba hadi Desemba mwaka huu ambapo zitaendelea na kwisha wiki ya nne ya Aprili mwaka kesho.
Kwa Nyanda za Juu Magharibi zinazojumuisha Mbeya, Songea, Iringa, Njombe, Ruvuma na kusini mwa Morogoro, mvua zitaanza Novemba hadi Desemba na kuendelea hadi wiki ya nne ya Aprili mwaka 2018. Dtk. Kijazi alitoa wito kwa wananchi kuyavuna maji yanayotokana na mvua hizo na kuweka chakula kwa ajili ya mifugo kwa vile mvua zitakuwa za wastani.

Source: Udaku.