TAARIFA YA KUIBIWA KIM KARDASHIAN YAMSABABISHA KANYE WEST KUKATISHA SHOW YAKE.

Kim Kardashian hatosahau tukio la Jumatatu hii pindi amevamiwa na watu wenye silaha kwenye jumba la kifahari alilokuwa amekodisha jijini Paris Ufaransa.

Majambazi hayo yalikuwa yamevalia sare za polisi. Msemaji wa polisi amedai kuwa mali zilizoibiwa zina thamani ya dola milioni 6.7. Vingi ni vidani vya madini.

Kanye-West

Watu hao walimfungia Kim bafuni na kupata muda mzuri wa kukusanya kila walichoweza kukibeba.

Tukio hilo limetokea saa nane na nusu usiku. Ripoti zinadai kuwa Kim ameshaondoka Ufaransa kwa kutumia ndege binafsi.

Wakati tukio linatokea, Kanye West, alikuwa jukwaani Meadows Music and Arts Festival New York na alipopewa taarifa aliwaambia mashabiki “I’m sorry, famil emergency. I have to stop the show.”

Tazama hii Video hapa

Story By: @Joplus_
Source: Perfect255.com