Siogopi Kutoa Nyimbo Wakati Wowote.

Belle 9 amesema hakuna kitu kinachoweza kumzuia kuachia wimbo wake hata kama kwenye muziki kuna kitu kikubwa kinaendelea. Muimbaji huyo toka Morogoro  kuwa anajiamini.

“Muda wote kwangu ni sahihi kwa kutoa ngoma haijalishi kuna kitu gani kinaendelea kwenye game wala kwenye soko iwe ndani au nje ya nchi,” amesema.

“Mimi nikiwa na ngoma natoa tu kwa sababu muziki ni kitu ambacho hakiingiliani na kitu chochote, yaani kwa mimi mtazamo wangu. So kwa mashabiki zangu wala wasidhani mi nitakuja kushindwa kutoa kitu eti kwasababu ya kitu fulani, No,” amesisitiza.

Source: Dizzim Online.