Kupitia kurasa za Instagram mwimbaji Shilole amefunguka kuhusu wanawake wanaojiita maboss Lady lakini hawana kitu huku wakiazima magari na kuishi kwenye nyumba za kupanga.
Shilole ameandika Pale unapojiita boss lady wakati unakaa nyumba ya kupanga na nagari ya kuazima! Mnanichoshaga nyinyi 😂😂😂😂 hebu watagi maboss lady uchwala tuwape vidonge vyaoooo bila kusahau link ya video ya kigori ipo kwa bio yangu” – Shilole.
Licha ya kuweka ujumbe huo kwenye Instagram yake Shilole hajamtaja mtu ingawa wapo warembo na mastaa wengi ambao wanajiita Boss Lady.
Source: Millard Ayo.