Real Madrid achezea kichapo

Antonio Sanabria alifunga bao la ushindi kunako dakika ya 94 huku Real Betis ikiishangaza Real Madrid na kupata ushindi katika uwanja wa Bernabeu kwa mara ya kwanza katika ligi ya Uhispania La Liga katika kipindi cha miaka 19 years.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 aliruka na kufunga kichwa kizuri kufuatia krosi iliopigwa na Antonio Barragans.

Kikosi cha Zinedine Zidane kilitawala kipindi kirefu cha mechi, lakini Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wa nyumbani waliopoteza fursa za kuiweka mbele Real Madrid huku klabu hiyo ikishambulia mara 27 bila kufaulu.

Hatua hiyo sasa inawawacha mabingwa hao wa Ulaya wakiwa pointi saba nyuma ya viongozi wa ligi Barcelona.

Ronaldo ambaye alikuwa amerudi kutoka kwa marufuku ya mechi tano alikuwa anashiriki katika mechi yake ya kwanza ya ligi msimu huu .

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale alimpatia Ronaldo fursa kabambe zaidi ili kuiweka mbele Real Madrid kwa kupiga krosi ya chini lakini mchezaji huyo wa miaka 32 akashindwa kucheka na wavu.

Luka Modric mapema alikuwa amepiga upande wa neti ya goli baada ya kutamba na mpira akiwa pekee huku shambulizi la Bale likiokolewa.

Na huku wakiendelea kutawala mechi, safu ya ulinzi ya Real Madrid ilipatikana imelala wakati bao la Sanabria lilipokataliwa na refa.

Muda mfupi baadaye kinda huyo wa zamani wa Barcelona hakufanya makosa wakati ambapo aliipata ngome ya Real Madrid ikiwa imezubaa na hivyobasi kufunga bao la ushindi na hivyobasi kuiweka Betis katika nafasi ya sita

story@moodyhamza