Ray C Sitaki muimbe nyimbo zangu.

Ray C amekataza kuimbwa kwa nyimbo zake kwenye tamasha la Fiesta linaloendelea nchi nzima. Jumapili hii alipost video inayowaonesha Nandy, Maua Sama, Ben Pol na Jux wakiimba wimbo wake Kama Vipi alioshirikiana na marehemu Mez B na kuandika:

Jamaani hii tabia sio nzuri kabisa!!! Sijafa bado! Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye show zenu muwe mnaniitaga basi!sina cancer ya koo ya Kushindwa kuziimba hizo nyimbo!Nandy hii mara ya mwisho ukipanda fanya kazi zako! Hii mara ya pili ujue! Mashabiki zangu hamuwatendei haki!i don’t like it sipendi! Maana hata tukigongana muda mwingine hata salam hamnipi kwahiyo staki mazoea…….
“Niliimba tusitaftiane visa tena Pisha sio tena Presha”😬😬
#sipendiunafki
#nawewetena
#mnanilakini
#kilamtuapaterizkiyakeyajasholake

Nandy alimjibu Ray C kwa kuandika:

Dadaangu Ray c, kama wote tulivyosema kabla ya kuimba juzi, mimi ni mmoja wa wasanii wanaokukubali kama mmoja wa wasanii waliotufungulia njia ya muziki wetu ulipo. Sitaacha kukuheshimu na kukubali kwa hilo wewe na wengine wengi tu. Siamini kukusifia na kukuenzi ni lizima uwe umekufa hapana siamini kwenye hilo sis nafanya jambo hili zuri kwa moyo wangu mzuri kama ulivyomuenzi Mama Mwanahela kwa nyimbo zake ulizorekodi za mahaba ya dhati na nimezama. Heshima yangu kimuziki kwako itabaki siku zote kama nilivo imba nyimbo za wengine nyimbo zao kama mwasiti, king kiki, yemi alade na recho.
🙏🏼🙏🏼🙏🏼 @rayctanzania

Hatua hiyo imedhihirisha kuwa Ray C hayuko vizuri na uongozi wa Clouds Media ambao ni waandaji wa tamasha hilo la kila mwaka.

Source: Teamtz.