Rapper Gucci Mane afunga ndoa.

 

 

Ni siku muhimu kwenye maisha ya rapper wa Marekani, Gucci Mane kwasababu ndio siku aliyofunga ndoa na mpenzi wake Keyshia Ka’oir.

Guccie Mane ambaye jina lake halisi ni Radric Delantic Davis, amefunga ndoa hiyo katika mji wa Miami, maeneo ya Four Seasons.

Harusi hiyo iliudhuliwa na mastaa kadha wakiwemo Diddy ‘Combs’, Kim Zolciak-Biermann, Karrueche Tran, Lil Yachty, 2 Chainz, Rick Ross, Big Sean na Jhene Aiko.

Source: Team Tz.