Rapa M.I Abaga Wa Afrika Kusini Amshtaki Nas.

Rapa mkali kutoka Nigeria M.I Abaga na lebo yake ya muziki ‘Chocolate City’ wameamua kumpeleka mahakamani rapa mkongwe Mmarekani Nas kwa kukiuka mkaubaliano ya mkataba wao wa kikazi.

M.I kupitia wakili wa studio, KC Okoli, amefungua mashtaka katika Mahakama Kuu ya New York kwa madai ya kuingia katika makubaliano na Nas pamoja mwenzake Ronnie Goodman mwaka 2013 ya kushiriki katika ushairi ya ubeti wa wimbo wa M.I ‘Man’ ambapo haikufanyika kulingana na makubaliano ndani ya malipo ya $50,000.

Katika makubaliano Nas alipewa jukumu la kuhakikisha katika ubeti wa wimbo huo anamtaja M.I, Chocolate City, Nigeria, Queens, New York, Mandela, Trayvon Martin, na mapambano ya Waafrika na Waamerika wa Kiafrika katika ubeti wake. Nas alifanya ubeti wake bila kutaja maneo husika yaliyotoka kama makubaliano kutoka kwa Chocolate City.

Chocolate City ikiwa ni lebo iliyokuwa na jukumu la kuhakikisha mambo yanenda kulingana na mkataba imedai fidia ya dola milioni moja kwa uvunjifu wa mkataba pamoja na dola elfu hamsini kwa usumbufu uliojitokeza.

Hata hivyo wimbo huo husika ambao ulihitaji ubeti wa Nas ulipaswa kuwa kwenye albamu ya M.I ‘The Chairman’ iliyoingia sokoni Oktoba mwaka 2014.

Source : Dizzim Online.