Patoranking Na Diamond Wafichua Siri.

Uvumi wa Staa na mkali wa ngoma ya ‘No Kissing Baby‘ kutoka Nigeria Patoranking kuwa anatengemea kupata mtoto katika siku za usoni umegeuka na kuwa katika sura nyingine ambayo inamhusisha pia Diamond Platnumz.

 

Kufuatia tetesi hizi Inakumbukwa kuwa zilisambaa picha katika mitandao ya kujamii kuwa kuna kitu kinachoeledelea kati ya Diamond Platnumz na Patoranking na baadhi waliobahatika kuona picha hizo ilianza kuhisikiwa kuwa kuna kazi ya pamoja inafaa tegemewa kutoka kwa wawili hao na baadae ilithibitika kuwa tarehe 1 Sepetemba wimbo wao utatoka rasmi.

Kupitia kionjo alichotuma Patoranking kupitia ukurasa wake wa instagram kimebadilisha tetesi za kuwa Patoranking sio kweli kuwa anategemea mtoto bali picha iliyotafsiriwa kuwa mrembo wake ni mjamzito ni moja ya kipande kilichopo katika video ya wimbo wake na Diamond Platnumz ‘Love You Die’.

Hata hivyo ngoma hii wengi watahisi hata wenigine kuamini kuwa imeshootiwa UK kwakuwa picha za wawili hao kuonekana kuwa wako location wakishoot video ya wimbo huo zilianza kusambaa kipindi cha safari na baada ya safari ya UK ya Diamond Planumz.

Source: DizzimOnline.