Nikki Wa Pili Azungumzia Maisha Yake.


Msanii Nikki wa Pili amesema maisha ambayo ameyapitia akiwa bado mdogo, ndio sababu inayomfanya azidi kufanya makubwa kwenye maisha yake.

Nikki wa Pili amesema alipitia changamoto nyingi ikiwemo kuuza sambusa kwenye vilabu vya pombe akiwa na baba yake, akiwa na umri mdogo kabisa.
“Nilikuwa nauza sambusa kwenye vilabu vya gongo na baba, kila siku nilikuwa nazunguka na sambusa zangu, nimefanya hivyo tangu nipo darasa la 3 mpaka namaliza la 7, lakini ndio hustle zilizotufanya tufanye makubwa zaidi”, amesema Niki wa Pili.
Niki wa pili ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya wa Kihasara, ni miongoni mwa wasanii wachache sana hapa bongo ambao wana elimu na upeo mkubwa wa kufikiri mambo, licha ya maisha duni aliyopitia.

Source: Udaku.