NICKI MINAJ AMFANANISHA JAY-Z NA KITABU CHA MAFANIKIO YA KIBIASHARA.

Rapper wa kike wa Marekani, Nicki Minaj amefanikiwa kukava jarida la Marie Claire la mwezi Novemba, mwaka huu.

Ndani ya jarida hilo, Nicki amezungumzia vitu vingi ikiwemo kushindanishwa na rapper wa kiume, kufanya kolabo na Beyonce, na mengine.

Rapper YMCMB, Nicki Minaj, mbali na hayo pia amesema kitendo cha kuyaangalia tu maisha ya Jay Z, ni somo kubwa la biashara kwake.

Amesema hayo kwenye mahojiano na jarida la Marie Claire.

Nicki-Minaj3

“Sihitaji kusoma kitabu kuhusu biashara, Naweza kumwangalia tu mtu fulani na kuona nini cha kufanya na kipi si cha kufanya na mtu pekee ambaye nimekuwa nikifanya hivyo katika maisha yangu yote ya muziki ni Jay Z,” amesema Nicki.

Kupitia account yake ya Twitter Nicki akatweet ujumbe huu “I promise if you trust me, I’ll lead you to greatness. Close your eyes & trust.”

“Alifanya kazi kubwa kutoka kuwa mtu wa mtaani hadi kuwa mfanyabiashara. Kwanini hakuna wanawake wanaofanya hivyo, kutoa mafanikio kwenye rap na kuanzisha himaya? Niliona kuwa chochote anachoweza kufanya naweza pia kufanya,” anasema rapper huyo.

Hizi hapa ni baadhi ya picha za kwenye Jarida hilo.

Nicki-Minaj4
Nicki-Minaj2

Story By:@Joplus_

Source: Perfect255.com