Nemo Amtumia Ommy Dimpoz.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye yuko chini ya Combinatin Sound, Nemo, amesema sababu ya kumshirikisha Ommy Dimpoz kwenye wimbo wake wa ‘Number One’ ni kutembea na upepo wa Dimpoz ambaye alikuwa juu kwa kipindi hiko ili kutafuta njia ya kutoka

Nemo amsema kwamba kwa hali ambayo alikuwa nayo kipindi kile ilimlazimu amtumie msanii kama Dimpoz, ili kutoboa kwenye game.

“Ilinibidi nimtumie Dimpoz kwa ajili ya trend ambayo ikikuwepo kipindi kile, na tayari alishajitengenezea njia kwa sababu Dimpoz ni msanii mkubwa ndani na nje ya nchi, kwa hiyo nikatembea na hilo”, amesema Nemo.

Hivi sasa Nemo ameamua kurudi kwenye game baada ya kimya kirefu, ambapo ameachia kazi mpya inayoitwa ‘kipotable’, inayoendelea kufanya poa kwa mashabiki.

Source: Udaku.