Mwanamuziki AY atangaza vita.

Rapper AY amesema hacheki na kima awamu hii. Amedai kuwa wale wote walioupload video ya wimbo wake na Mwana FA na Fid Q, Upo Hapo wanajitafutia matatizo makubwa.

AY amesema amesikitishwa na kitendo hicho kwakuwa gharama, muda na nguvu vimetumika kuandaa video hiyo.

Wamesema wamiliki wa video hiyo, Mkito walifile complain Youtube ili wale wote walioweka video hiyo waitoe, ajabu wapo waliojibu kwa kusema ni video yao, kitu ambacho kimewaudhi zaidi.

Kutokana na hilo, AY amesema watawasaka wote waliofanya hivyo ili kuwafunza adabu.

Source: Dizzim Online.