Mwanafunzi wa Darasa la Saba Kenya Ajifungua Dakika Chache kabla ya Mtihani na kufanya mtihani

Jana November 1 Wanafunzi wa Darasa la nane Nchini Kenya wameanza mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi huku Vikitokea Vimbwanga viliwili vya Wanafunzi waliojifungua Masaa machache kabla ya Mtihani.

Sio Tanzania tu ila hata Kenya bado vitendo vya Watoto Kubeba mimba Mashuleni Vinaendelea na Jana Wanafunzi hao wameidhihirishia Dunia kwamba wao Hawashindwi Kuwa Kinamama wakiwa Shule ya Msingi.

Wanafunzi wakifanya Mtihani wa mwisho KCPE
Wanafunzi wakifanya Mtihani wa mwisho KCPE

Mwanafunzi mmojawapo anatoka Shule ya Msingi  Lenana inayopatikana Mjini Narok ambapo yeye alilazimika Kufanya Mtihani wake akiwa Wodini hospitali baada ya Kujifungua Mtoto Masaa matano kabla ya Mtihani.

Msichana huyo mwenye Miaka 13 tu ilibidi apewe Msimamizi Maalum wa Mtihani na Kusimamiwa kufanya Mitihani yake akiwa Ward ya kujifungua na hata leo ameendelea na Mitihani yake.

Mwanafunzi akifanya Mtihani Chumba cha kujifungulia baada ya kujifungua Masaa machache kabla ya Mtihani
Mwanafunzi akifanya Mtihani Chumba cha kujifungulia baada ya kujifungua Masaa machache kabla ya Mtihani

Kwenye tukio lingine Mwanamke mwenye miaka 30 ambaye anasoma shule ya msingini huko Siaya alijifungua Dakika Chache kabla ya kuanza mtihani wake wa Darasa la saba katika Hospitali ya Wilaya ya Bondo kwa mujibu wa Citizen TV.

Kwa  mujibu wa Citizen digital Mwanamke huyo alilazimika Kuanza Mtihani wake Dakika 45 baadae tena kwa kulazimishiwa kwani bado alikuwa Chumba cha kujifungulia hivyo badala ya kuanza mtihani wake saa mbili kamili asubuhi akalazimika kuanza Mtihani saa mbili na dk.45.

Naye amepewa usimamizi maalum kwa Nchi hiyo inaamini Kila mtu ana haki na elimu na Ujauzito hauumzuii mwanafunzi wa Shule ya Msingi kufanya Mtihani.