Mtu wa kwanza kutumia neno SALAFI ni mtume صل الله عليه وسلم alipomwambia mwanae bi Faatima رضي الله

منهج الأنبياء:
NINI MAANA YA SALAF

Neno سلفي (salaf) linakusudiwa Wema waliopita na Al muhimu ni Wanafunzi na wafuasi wake mtume صل الله عليه وسلم yaani SALAFI ni MASAHABA

➡️ Mtu wa kwanza kutumia neno SALAFI ni mtume صل الله عليه وسلم
alipomwambia mwanae bi Faatima رضي الله عنها

“فاتقي الله واصبري فاءنه نعم السلف انا لك”

“Mche Allah na kuwa na Subra kwani mi ni Bora katika Salafi kwako”

————————-
Sahih Bukhaary – Mjeredi wa 8 hadith ya 58885 📚
Neno salafi limetumiwa sana na WANACHUONI kuanzia wa Kale mpaka baadhi wa zama za leo

Mfano IMAM AHMAD Ibn HAMBAL رحمه الله

IMAM ABU HANIFAH na wengi katika wao.

➡️ Salafiyyah (wanaofuata Mafundisho ya mtume kama walivyofahamu masahaba zake) Huitwa pia AHLU HADITH, AL ATHARI, AHLU SUNNAH WAL JAMAA na mfano wake

DAAWA YA SALAFI IMESIMAMIA MISINGI GANI?

➡️ Kufuata Aqeedah (ITIKADI) mambo yaliyofungamana na imaan kama Alivyofundisha mtume na ufahamu wa masahaba

➡️ Kushikamana na Sunnah vilivyo katika kila Ibaada na kujitendea

➡️ Salafiyyah ni watu wanahimiza sana TAWHIID na kukaa mbali kbs na Shirk kwa nguvu zote

➡️ Salafiyyah huwaigiza Mtume na masahaba zake tabia zao njema walizoshikana nazo

➡️ Manhaj (njia yao Mtume na masahaba)

……………………….

kwanini mtu afuate Manhaj SALAFI ni kwa sababu zifiatazo

DALILI katika QUR’AN

Allah Jalla wa’ala amesema

فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِلْآخِرِينَ

Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye…

Az Zukhruf : 56 📚
——————————

فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنْتُمْ بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوْا ۖ وَإِنْ تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Basi wakiamini kama mnavyo amini nyinyi (Kundi la Masahaba na mtume), itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni na shari yao, na Yeye ndiye Msikizi, Mjuzi….

Al Baqarah : 137 📚

—————————–

 

KWANINI UFUATE MASAHABA (SALAFI) ufahamu wao kwa kila JAMBO?

 

dalili katika sunnah

Amesema mtume صل الله عليه وسلم

“خير الناس قرني، ثم الزين يلونهم، ثم الزين يلونهم”

“Watu bora kabisa ni Karne yangu (masahaba) kisha wataofuata (tabiin) kisha karne itakayofuata (at’bau Tabiin)

Imepokewa na Bukhaary📚
———————————

Amesema Mtume صل الله عليه وسلم

“وانه من يعش منكم فسير ي اختلافا كثيرا

Yeyote atakayeishi muda mrefu baada yangu ataona Makasoro mengi katika dini hii

فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين

“”Shikamaneni na sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa wangu waongofu”

story@moodyhamza