Msaga Sumu Atoa Yamoyoni.


Mfalme wa singeli nchini Tanzania, Msaga Sumu amefunguka na kudai wasanii wengi wa singeli wanatapotea katika muziki kwa sababu ya kutokuwa na heshima kwa watu wanaowazunguka kwenye kazi zao.

Msaga Sumu amebainisha hayo baada ya kupondwa kwa maneno makali kwa kipindi kirefu na wasanii wenzake huku wengine wakimwambia hajui lolote katika muziki huo anaouimba.
“Wasanii wa singeli mimi naamini wananiponda sana, tena nikikaa kimya hivi ndiyo wanasema nimefulia kabisa, kumbe mwenzao huwa najitungia sheria zangu huku nikiwaangalia wao. Lakini huwa nawaambia ukweli kwamba siku zote kwenye muziki ukiwa na heshima unaweza kufika mbali, kwa kuwa heshima ndiyo kila kitu. Lakini hawa wasanii wa singeli wengi watafeli kwa sababu heshima hawana, wanajifanya wanavimba kutokana na nyimbo zao moja moja walizokuwa nazo”, amesema Msaga Sumu.

Source: Udaku.