Mr Blue Azungumzia Ndoa Ilivyombadilisha.


Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Mr Blue amefunguka na kusema toka ameoa mke na kuwa na familia imemsaidia sana kubadili maisha yake na kumfanya aachane na mambo ya kijinga ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya kuoa.

Mr Blue afunguka na kusema kuwa ndoa imemfanya kuwa kijana mwema mwenye kutambua majukumu ya ndoa na kulea familia yake na kuachana na mambo mengine ya hovyo hovyo ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya kuoa.

Msanii huyo aliendelea kueleza kuwa wakati yupo kwenye uchumba na mkewe huyo bado alikuwa na mabinti wengine kadhaa ambao alikuwa anatoka nao kimapenzi lakini ilifika hatua aliamua kuoa na kutulia na mkewe wa ndoa.

Source: Udaku.