Mose Iyobo azungumzia mipaka ya kuigiza aliyomuwekea Aunt Ezekiel

Dancer wa WCB ambaye pia ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo movie Aunt Ezekiel, Mose Iyobo amefunguka kukubaliana na mpenzi wake huyo kuwa hakuna haja ya kulala kambini wakati wanatengeneza movie bali anatakiwa kurudi nyumbani kila wakimaliza kupiga picha.

Iyobo amezungumza kupitia 255 ya XXL May 25, 2017 na kusema hakuna haja ya Aunt Ezekiel kulala kambini kwa sababu hata hizo scene ana-shoot mchana hivyo ni vizuri arudi nyumbani na hakuna haja ya kulala huko.

>>>“Mwanzoni hiyo hali ilikuwa inaniumiza lakini tulipokubalina kuwa mimi ni baba na yeye ni mama basi vitu vya kambini vikaisha. Kama anaenda ku-shoot siku nzima, aka-shoot na ahakikishe anarudi nyumbani lakini sio kulala huko huko.

“Utalalaje huko wakati una nyumba? Halafu kama ku-shoot hafanyi hivyo asubuhi, sasa kwa nini akalale kambini. Ni kweli haamki mapema, anaamka karibu saa 6 mchana kwa hiyo ni bora alale nyumbani asubuhi aende kazini. Ni wivu tu wa mapenzi na wasiwasi ndio akili sasa kwa nini akalale huko?” – Mose Iyobo

Source: Millard ayo