Mo Music azungumzia kolabo alizofanya nje.

Staa kutoka katika kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva Tanznaia ‘Moshi Katemi’ a.k.a Mo Music anayefanya vyema na ngoma yake ‘Usiniache’ aliyomshirikisha Barakah The Prince, amezungumzia ngoma alizojipanga nazo kwa lengo la mfululizo wa kuziachia moja baada ya nyingine katika hatua za kubadilisha mfumo wake wa kukaa kimya kwa muda na kuchelewa kuachia ngoma.

Mo Music amesema kuwa ni kweli mfumo wa kazi zake umekuwa hautabiriki kwa maana kuachia nyimbo kipindi ambacho kinaacha muda mrefu kiasi cha mashabiki kusubiria sana ambapo sasa amewahakikishia mashabiki kuwa baada ya kuachia hii kolabo yake mpya atachia kazi kwa mfumo wa kutoacha nafasi kubwa ya mashabiki kusubiria na kuzungumzia ngoma alizofanya na wasanii wa ndani na nje ya Tanzania.

Source: Dizzim Online

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors