Lulu Diva Awapa Makavu Wenzake.

Msanii wa bongo fleva Lulu Diva ameibuka na kuwachamba watu wanaomuongelea vibaya juu ya vitu vya gharama na magari anayotumia kuwa ni ya kuazima kwa kusema kwamba wengi wanaomzungumzia wana maisha duni .

Lulu amesema yeye ni mtafutaji hivyo siku zote anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba anaishi maisha anayohitaji na siyo kuigiza maisha kama jinsi watu wanavyomfikiria.
‘Niseme tu ukweli Lulu anaishi maisha yake halisi na kila kitu ambacho unakiona kwa Lulu Diva ni mali yangu sina tabia za kuazima vitu, mimi ni mtafutaji na natumia mda wangu mwingi kuhangaika kutafuta vya kwangu sipendi kuigiza maisha”aliongea Lulu

Hata hivyo Lulu aliendelea kusema kuwa kwa upande wa magari kuna wakati natumia magari ya menejiment yangu ambayo ni kama magari ya office ninayofanyia kazi na sioni tatizo na hilo kwa kuwa mimi nafanya kazi na pia ni mmiliki wa baadhi ya magari ninayotumia.
Pia Lulu aliendelea kusema kuwa hajali maneno ya watu wanayoyaongeaa juu yake kwani anachikifanya ni kuhakikisha anawaziba midomo wote wanaomsema vibaya kuwa anaanzima vya watu na waamini kile anachokifanya maishani mwake.

Source: Udaku.