Kutana na AB CLASSIC Msanii Mchanga mwenye Kipaji cha Kina Kiba na Diamond

Hakika moja ya kazi kubwa Tuliyonayo watu wa Media ni kuwafikishia Bidhaa mpya za mioyo yenu ambazo ni Burudani ya moyo.

Leo nimeona nikusogezee kijana Mpya kwenye Game ya Bongo Fleva ila uwezo wake ni kama Mkomavu kwenye Muziki

ab-classic-tatizo-nyota-mp3

Jina la Kuzaliwa anaitwa Ayoub Kyando kwenye Muziki anajiita AB Classic akitokea Mkoa Mpya wa Njombe.

Huu hapa ni wimbo wake Mpya ambao anaupa heshima ya kufika kwa Walaji wa muziki Mzuri.

Wimbo wenyewe ameupa jina la TATIZO NYOTA Ukiwa umetengenezwa na Producer Bora Defxtro Maarufu kama DX wa NoizMekah Studio Arusha Tanzania.

ANACHOKIHITAJI KWAKO NI SUPPORT KWA KUUPIGA WIMBO WAKE, AU KU-SHARE KWA WADAU