Kuhusu taarifa za Haruna Niyonzima wa Yanga kutoonekana nchini

Jumamosi ya March 11 uwanja wa Taifa timu ya Dar es Salaam Young Africans watacheza mchezo wao kwanza wa round ya pili wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC ya Zambia, taarifa ikufikie kuwa Zanaco FC wamewasili leo wakitokea Zambia lakini maswali yamekuwa mengi mtaani.

Haruna Niyonzima

Hususani kwa mashabiki wa Yanga kuhusu stori za nahodha msaidizi wa Yanga Haruna Niyonzima kutokuwepo kambini, shida nini? na ni kweli hayupo kambini? katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa na kocha msaidzi Juma Mwambusi wameeleza sababu za kukosekana kwa kiungo huyo kambini.
“Suala la Haruna ni kwamba aliomba ruhusa ya kwenda kutengeneza passport yake kwao Rwanda ilikuwa imejaa kabisa na haikuwezekana kumtengenezea passport yake akiwa hapa, kwa hiyo aliomba ruhusa akaruhusiwa kwa hiyo ameenda kuishughulikia”
                                                 SOURCE BY:MILLARD AYO